Wasiofanya usafi kesho kuchukuliwa hatua kali
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Mecky Sadiki amewataka wakazi wa jiji Dar es Salaam kujitokeza kufanya usafi hapo kesho kama ilivyotangazwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku ya Uhuru Desemba 9, itumike kufanya usafi badala ya kusherehekea vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

