Frasha apiga vita ulevi Kenya
Star wa muziki Frasha kutoka kundi la P-Unit Kenya, amejikita katika kampeni ya kupambana na utumiaji wa pombe ambao umekuwa na athari kwa kiasi kikubwa katika jamii, akiwa binafsi amekamilisha lengo la kukaa siku 40 bila kunywa.