Serikali yasitisha zoezi la bomoabomoa Morogoro
Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Morogoro imesitisha rasmi zoezi la ubomoaji wa nyumba lililokuwa likifanyika katika eneo la CCT Forest kata ya Mkundi katika manispaa hiyo baada ya kuibuka hali ya sintofahamu kwa baadhi ya nyumba kubomolewa.
