Straika wa JKT Ruvu amfunika Donald Ngoma
Mshambuliaji Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi Mei 2016. Mussa katika kinyag'anyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting.