Watanzania watakiwa kuzingatia afya ya kinywa
Watanzania wametakiwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara, ikibidi angalau mara moja kila mwaka ili kuondokana na tatizo la milipuko ya magonjwa yakiwemo yanayohusu afya ya kinywa na meno, ambayo yameendelea kuwaathiri watu wengi.