Watu milioni 25 Tanzania wameambukizwa kifua kikuu
.jpg?itok=CXk4zLf6)
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisaini Maazimio ya Wabunge wa Tanzania yenye dhamira ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu" TB Caucus ",mtandao huo ulianzishwa jijini Barcelona, Hispania Oktoba 2014 na kuitwa Mtandao wa Wabunge duniani "The Global TB Caucus
Takwimu zinaonesha ya kuwa, takribani asilimia kati ya 30 na 50 ya watanzania wote tayari wameambukizwa Kifua kikuu, yaani watu wapatao million 25 hali inayotishia ukuaji wa uchumi wa taifa na shughuli za maendeleo.