Miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa shemeji yake
Mkazi mmoja wa kijiji Mwanundi kilichopo kata ya Seng'wa wilayani Maswa mkoani Simiyu aliyefahamika kwa jina la Luth Jacob (50) amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mtoto wa shemeji yake.