Mashinji aweka wazi kuhusu kuhamia CCM
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Vicent Mashinji amekanusha habari za kwamba anahamia Chama cha Mapinduzi na kusema kwamba yeye siyo mtu wa kuamini kwenye zidumu fikra za Mwenyekiti bali nguvu ya mamlaka ya umma.