Nyota wa Tanzania kupata shavu Afrika Kusini
Baada ya tetesi kwamba Deus Kaseke huenda akaungana na kocha Hans Van Pluijm pamoja na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United kujiunga Azam, Mkurugenzi wa Singida United amesema Kaseke atatimkia Afrika ya Kusini ambako amepata ofa.