Rasmi Ufaransa yatambua uwepo wa Palestina
Makofi mengi yamesikika wakati Ufaransa ikilitambua taifa la Palestina siku ya jana Jumatatu, Septemba 22 na kuushinda msukumo wa miezi kadhaa wa utawala wa Trump uliokuwa ukizikatisha tamaa nchi nyingine kuungana na Paris katika mpango huo.