Lema azungumzia Zitto kufuatiliwa na wasiojulikana
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema juzi Jumatano Februari 6, 2019 walilazimika kumuondoa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe baada ya kufuatiliwa na watu ambao hakuwataja.

