Bashe afunguka baada ya kuteuliwa na Rais
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amemshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na kueleza kuwa atahakikisha anakuwa msaidizi wa mwema wa Waziri Japhet Hasunga ili kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele.