Fahamu historia ya Lampard ndani ya Chelsea
Frank Lampard ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Chelsea, kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea klabu ya Derby County ambayo ilicheza 'Play off Final' ya kuingia EPL lakini ikafungwa na timu ya Aston Villa ambayo kocha msaidizi ni mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea John Terry.