DC atuhumiwa kuomba rushwa ya Mil 5
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amejibu madai ya kuomba rushwa ya Mil. 5 yaliyotolewa na mmoja wa wafanyabiashara wa Hoteli za Kitalii mkoani Kilimanjaro, katika mkutano wa wadau wa Utalii mkoani humo, ambapo Sabaya mwenyewe amedai suala hilo limeanzia kwenye mgogoro wa ardhi.