Aliyemtapeli DC Jokate adakwa na TAKUKURU
Mkazi wa Chamazi Omary Chuma, leo Julai 10, 2019 anatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Pwani, kwa kosa la kumtapeli mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, baada ya kujifanya ofisa wa Serikali.