Morogoro: Mavuno yaleta ubakaji
Imeelezwa kuwa katika kipindi cha mavuno, matukio ya ubakaji kwa wanawake na wasichana hujitokeza zaidi mkoani Morogoro, huku chanzo kikielezwa kuwa ni uwepo wa ngoma za kienyeji zinazochochea ulevi uliokithiri hivyo wanaume wengi kuingiwa na tamaa za kimwili.