Ufaulu kidato cha 6, Asilimia 97.58 hadi 98.32
Baraza la Mitihani la Taifa limetoa pongezi kwa walimu, Maafisa elimu kwa kusimamia vizuri kazi ya ufundishaji na kufanikisha kwa kiasi kikubwa, shule zote nchini kufanya vizuri, ambapo ufaulu umeongezeka, kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018, hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019.