Ajikata koromeo baada ya kumuua mkewe
Mkazi wa Kijiji cha Kagera wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, Celestin Masatu (39) amefariki dunia baada ya kujichoma na kisu na kisha kujikata koromeo, ikiwa ni saa chache tu baada ya kumchomachoma mke wake na kisu mwilini.

