NEC yashangazwa na majibu ya DED Ubungo
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Athumani Kihamia, ameshangazwa na kauli ambayo si ya kweli iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, baada ya kugoma kumuapisha diwani aliyeteuliwa na Tume hiyo, kwa madai ya kwamba hajapokea barua ya uthibitisho,

