Makonda aja na jipya kuhusu watoto wa nje ya Ndoa
Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda, amesema atawasilisha muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya mirathi na sheria ya Ndoa kwa Waziri wa Katiba na Sheria, ili ziweze kufanyiwa marekebisho kutokana na sheria hizo kupitwa na wakati.

