Rais Magufuli atuma salamu ajali ya moto Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameungana na watanzania wote kutoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza ndugu zao, katika ajali ya moto iliyotokea eneo la Msamvu Mkoa wa Morogoro, baada ya Lori kuanguka na kulipuka moto.