Tundu Lissu asogeza mbele tarehe ya kurudi TZ
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amesema amesogeza mbele tarehe ya kurudi Tanzania, kutokana na daktari wake kumtaka kuonana naye tena mwanzoni mwa mwezi Oktoba, kwa ajili ya matibabu ya mwisho.