Mtolea aeleza ushiriki wake, kwenye sakata la Meya
Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea, amesema yeye ni miongoni mwa wajumbe ambao wamesaini hoja ya kutokuwa na imani ya Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, ambaye mwenyewe anatarajiwa kuwasilisha utetezi leo kwa Mkurugenzi.

