Mkuu wa Wilaya akomaa na wahasibu waliopiga pesa
Sakata la upotevu wa kiasi cha Shilingi Milioni 76 za ada ya wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Moshi, lililopelekea wanafunzi hao kuandamana, limeleta sura mpya baada ya Bodi ya Shule, Benki ya CRDB na Mawakala wa benki hiyo kukaa na kuweka makubaliano ya kwamba kila mmoja awajibike.

