Polepole aagiza Mil 200 zitengwe kwa vijana/wamama
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) taifa, Humphrey Polepole, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Modest Alpolnary, kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya vijana na Wanawake mkoani Geita.

