Anayedaiwa kumuua mkewe, aomba laini kutoa pesa
Mfanyabiashara Hamis Said (38), anayekabiliwa na kesi ya kumuua mkewe, Naomi Marijani, leo Agosti 27 ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumpatiwa laini zake mbili za simu zenye zaidi ya Shilingi Milioni 5 ili azitoe pesa hizo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake na ada ya mwanaye.