Ukweli kuhusu wanafunzi 1129 kufeli UDSM
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii juu ya matokeo ya mitihani ya wanafunzi chuoni hapo, inayodai kuwa takribani wanafunzi 1129 wamefeli 'disco' kuendelea na masomo huku wengine zaidi ya 7000 wakitakiwa kurudia mitihani.