Kabendera aileza Mahakama majibu ya vipimo
Leo Septemba 18, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeendelea kusikiliza kesi ya Mwandishi wa Habari Erick Kabendera, anayekabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la Uhujumu uchumi, ambapo ameieleza Mahakama kuwa baada ya kufanyiwa vipimo amekutwa na matatizo ya mgongo.

