Uenyekiti wa Mbowe kwisha, Msajili ampa siku 7
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,imesema kuwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, umemaliza muda wake tangu Septemba 14, 2019 na hivyo walipaswa kufanya mkutano wa kuchagua viongozi wengine.

