''Kuna njama ovu, Tanzania haina Ebola'' - Ummy
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu, amewataka watanzania kuzipuuzia taarifa za uongo, zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwa madai ya kwamba Tanzania imekuwa ikificha taarifa za uwepo wa ugonjwa wa Ebola hapa nchini.

