Muuguzi aliyebaka hospitali, leseni yake yafungiwa
Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Tanzania, limeisimamisha kwa muda wa miezi mitatu leseni ya muuguzi, aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka, msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyekuwa akimuuguza mama yake, katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

