Mbabe wa Madrid aongezewa mkataba Barcelona
Kocha Hansi Flick anatarajia kusaini mkataba mpya Barcelona hadi Juni 2027. Flick amefanya mapinduzi makubwa Barcelona tangu alipowasili majira ya joto yaliyopita ikiwemo kuchukua ubingwa Super Cup Spain na Copa del Rey kufuatia kufukuzwa kwa Xavi Hernandez.