Askari waliomfyatulia risasa muuza barakoa Kenya
Maafisa wawili wa polisi waliomshambulia na mmoja wao kumfyatulia risasi kijana aliyekuwa anauza barakoa siku ya maandamano ya kupinga mauaji ya kijana Albert Ojwang aliyefia mikononi mwa polisi nchini Kenya, wataendelea kuzuiliwa na polisi kwa siku 15 zaidi huku uchunguzi ukiendelea.