Bandari kavu, Kongani ya viwanda kukuza uchumi
Kwa mujibu wa Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara, mradi huo mkubwa unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 150,000 kwa Watanzania. Tayari watu 311 wamekwishapata ajira kupitia shughuli zinazoendelea hapo.