RUWASA yatakiwa kufikisha maji vijiji vyote nchini
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ametoa wito kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kufikisha huduma ya majisafi ya bomba katika vijiji takribani 1,500 vilivyobaki ifikapo mwaka 2030 ili huduma hiyo ipatikane katika vijiji vyote 11,353 vilivyo chini ya wakala huo