Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mkoani Mwanza
Kivutio kikubwa kutoka burudani zilizojiri siku ya leo ni onesho kutoka kwa msanii mwenye uwezo mkubwa wa kughani mashahiri, Mrisho Mpoto ambaye kupitia onesho lake akishirikiana na Ismail, alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wafanyakazi kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Ikafuata Hotuba ya Rais, ambapo katikati yake akaonesha uwezo kidogo na kutoa kauli kuwa pembeni ya uongozi, fani yake ingekuwa kuimba.
"Nisingekuwa Rais ningekuwa Bongo Flava,.... hata kama nisingeweza kuwashinda akina Diamond na Ali Kiba lakini rekodi zangu zingeuza pia"