Ijumaa , 24th Apr , 2015

Uongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA, umeandaa kozi ya waamuzi inayotarajiwa kufanyika Aprili 28 mpaka Mei mbili mwaka huu jijini Dar es saalaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Mjumbe wa kamati ya maandalizi na ufundi wa DAREVA, Nassoro Shariff wameandaa kozi hiyo ili kuweza kupata waamuzi watakaoweza kuchezesha mashindano mbalimbali.

Shariff amesema, wamepeleka mialiko kwa vilabu vyote vya mkoa wa Dar es salaam na wanasubiri majibu ili kuweza kupata idadi ya washiriki wa kozi hiyo.

Kwa upande mwingine, Shariff amesema, mzunguko wa pili wa ligi ya wavu mkoa wa Dar es salaam unatarajia kuanza Mei tisa mwaka huu..