Ijumaa , 10th Apr , 2015

Shirikisho la Soka nchini TFF limesema watahakikisha wanafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya Timu ya Taifa inayotarajia kushiriki michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika pamoja na Fainali za Michuano ya wachezaji wa ndani CHAN Juni mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema, michuano ya COSAFA itakayofanyika mwezi wa tano katikati mpaka mwishoni itasaidia timu kuweza kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya CHAN na Mataifa ya Afrika.

Kizuguto amesema kwa upande wa michuano ya Mataifa ya Afrika hawahofii sana kuwa kundi moja na Nigeria, Misri na Chad kwani wanaamini lolote linawezekana kutokana na maandalizi kwani mshindi atakayepatikana ataweza kusonga mbele.