Kupitia majibu aliyotoa baada ya kuulizwa sana na watumiaji wa mtandao huo, Mosseri amesema kuwa ili maudhui yako yafikie watu wengi zaidi, njia bora ni kujibu maoni (comments) ya watu na kushiriki kwenye mazungumzo (engagement) na wafuasi wako.
Kwa mujibu wa Mosseri, ushiriki wa moja kwa moja kati ya mtayarishaji wa maudhui na wafuasi wake huonyesha kuwa kuna thamani na mwingiliano wa kweli, jambo linalochangia sana maudhui kuonekana zaidi kupitia algorithm ya Instagram.




