Vinicius Jr na Xabi Alonso
Kulingana na gazeti la The Athletic, ameifahamisha Los Blancos kwamba hataongeza mkataba wake wa sasa huku uhusiano wake na kocha mkuu Alonso ukiendelea kuwa mbaya.
Kutengana baina ya wawili hao kuliingia kwenye vichwa vya habari wakati Madrid waliposhinda mechi ya Clasico dhidi ya Barcelona mapema msimu huu. Vinicius alionekana kufoka baada ya kutolewa nje na Alonso katika kipindi cha pili cha mechi.
Baadaye aliomba radhi hadharani kwa tabia yake lakini aliibua hisia zaidi kwa kutomtaja meneja wake katika taarifa yake
Mkataba wa Vinicius unamalizika 2027 na bado hajafikia makubaliano na klabu ya kuongeza muda wake wa kusalia.




