Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza Baraza jipya la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika tangazo hilo, Rais Mwinyi ametaja majina ya Mawaziri 16 kati ya wizara 20, huku wizara nne akiziacha wazi kwa ajili ya chama cha upinzani, ACT Wazalendo, endapo kitakubali kushiriki katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Rais amesema kuwa atatangaza mawaziri wa wizara hizo mara baada ya chama hicho kutoa taarifa rasmi ya ushiriki wao.
Orodha hii ya Mawaziri imetolewa leo Novemba 13, 2025, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar, mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.

