Jumatatu , 18th Aug , 2025

Rais Donald Trump jana Jumapili alidokeza kwa ufupi ujumbe atakaoutoa kwa wageni wake wa Ikulu ya White House mojawapo ikiwa ni pamoja na Zelensky lazima akubaliane na baadhi ya masharti ya Urusi ili vita vya Ukraine vikome.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewasili nchini Marekani usiku wa kuamkia leo Agosti 18, 2025 ambapo anatarajiwa kuzungumza na Rais Donald Trump kuhusu mustakabali wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.

Kuelekea mazungumzo yenye matokeo muhimu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na ujumbe mkubwa wa viongozi wa Ulaya, Rais Donald Trump jana Jumapili alidokeza kwa ufupi ujumbe atakaoutoa kwa wageni wake wa Ikulu ya White House mojawapo ikiwa ni  pamoja na Zelensky lazima akubaliane na baadhi ya masharti ya Urusi ili vita vya Ukraine vikome.

CNN imenukuu Trump akisema kuwa “Rais Zelenskyy wa Ukraine anaweza kumaliza vita na Urusi karibu mara moja, ikiwa anataka, au anaweza kuendelea kupigana. Kumbuka jinsi ilivyoanza. Hakuna kurudia Obama alivyopewa Crimea (miaka 12 iliyopita, bila risasi kufyatuliwa!), na HAKUNA KUINGIA NATO KWA UKRAINE. Mambo mengine hayabadiliki!!!”

Wakati Viongozi wa Ulaya na NATO wakitangaza mara moja kuwa kuungana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Washington kuwasilisha msimamo mmoja katika mazungumzo na Rais wa Marekani Donald Trump juu ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine na kuimarisha dhamana ya usalama ya Marekani sasa kwenye meza ya mazungumzo, Jenerali mstaafu wa Ufaransa Dominique Trinquand, mkuu wa zamani wa ujumbe wa kijeshi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa amesema EU wanaogopa sana tukio la Oval Office kurudiwa na kwa hivyo watamuunga mkono Bw. Zelensky kwa kilele.