Alhamisi , 26th Jun , 2025

Kwa zaidi ya Miaka saba sasa Game ya muziki wa #BongoFleva imeshindwa kuzalisha wasanii wapya wakubwa ambao tunaweza kujivunia kama wasanii wetu wapya wakubwa.

Ukitoa Kizazi cha wasanii kama Diamond Jux Ben Pol Belle 9 Rich Mavoko ambao walitoka pamoja kimuziki ama kwa kupishana mwaka mmoja mmoja na wote wakasimama mpaka leo wanatajwa kuwa wasanii wakubwa

 

Kizazi kinachofuata hapa ni kizazi cha kina Nandy Marioo Jay Melody Mbosso Lava lava wametoka zaidi ya miaka saba, kinafuata kizazi cha Zuchu Ibraah ambao wao pia wametoka miaka mitano iliyopita na mpaka leo wanatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa kiwandani.

 

Sasa kwa zaidi ya miaka Minne sasa game ya Bongo Fleva imeshindwa kuzalisha wasanii wapya wakubwa kulinganishwa na hao tajwa hapo juu,wanatoka wasanii wanafanya vizuri ngoma mbili tatu kisha wanapungua makali jambo ambalo ni tofauti kwa viwanda vingine kama singeli imekuwa ikizalisha wasanii wapya na wakubwa kila baada ya muda