
Msemaji wa WHO Dkt. Margaret Harris amesema kuwa ukanda wa Gaza unashuhudia mashambulizi mara kwa mara katika hospitali na wahudumu wa afya.
Kuna uhaba wa vifaa vya matibabu kufuatia Israel kuzuia wafanyikazi wa hospitali ya Al Ahli iliyoko mjini Gaza siku ya Jumapili ambapo kombora la Israel lililenga maabara ya hospitali na kuharibu chumba cha dharura.
Hata hivyo hakuna waathirwa wameripotiwa kufuatia shambulizi hilo ila kuna mtoto aliyefariki baada ya sintofahamu kutokea katika uangalizi wake.
Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Uingereza lilisema Jumatatu kwamba wameshtushwa na kwamba hospitali zinageuzwa kuwa uwanja wa vita huko Gaza, na kwamba Israeli bado haijatoa ushahidi wa wazi na wa kuridhisha kuthibitisha madai yake kwamba Hamas ilikuwa ikitumia hospitali hiyo.
Usitishaji vita huko Gaza ulimalizika wakati Israel ilipoanzisha tena mashambulizi ya anga na ardhini wiki nne zilizopita, ikisema shinikizo la kijeshi litailazimisha Hamas kuwaachilia mateka ambao bado inawashikilia.