Jumanne , 11th Mar , 2025

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Sebastien Haller ameitwa katika kiosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya kukosekana katika madirisha matatu ya FIFA yaliyopita kutokana na majeraha

Sebastien Haller - Mshambuliaji wa Borussia Dortmund

Nyota huyo ambaye anaitumikia FC Utrecht kwa mkopo ataiwakilisha  Ivory Coast katika mechi za kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 dhidi ya Burundi na Gambia wiki ijayo.

Mbali na Haller nyota wengine waliorejea katika kikosi hiko ni kiungo wa Nottingham Forest Ibrahim Sangare, Jean-Philippe Gbamin huku nyota wa Manchester United Amad Diallo na Wilfried Zaha wanaendelea kukosekana kwa sababu tofauti tofauti.