
Sasa kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa nchini Ujerumani na kuchapishwa katika jarida la 'computer in human behavior' ulionesha kwamba usipotumia simu yako ya mkononi kwa angalau siku tatu hupelekea mabadiliko kwenye ubongo wako (ubongo unavyofanya kazi na muundo wake)
Utafiti huo uliojumuisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 -30, wakati wa utafiti walichukuliwa wataalamu wa kipimo cha uchunguzi ndani ya mwili (MRI) na wataalamu wa saikolojia ambao walikuwa wakichunguza mabadiliko kwa watu waliositishiwa matumizi ya simu kwa muda wa saa 72
Matokeo ya tafiti hiyo kuonesha kwamba kuachana na simu yako kwa siku tatu kunaweza kubadilisha kwa kina muundo wa ubongo wako.