Jumapili , 2nd Mar , 2025

Barcelona wanatazamia kumuongezea mkataba Raphinha ukiwa na kipengele cha kumuuza baada ya Kombe la Dunia la 2026 kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Uhispania.

Raphinha - Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi wa Barcelona wa msimu huu, akifunga mabao 24 na kusaidia (assists)18 katika mechi 38 katika mashindano yote.

Klabu za Premier League na Saudi Pro League zimetajwa kuhitaji huduma ya Raphinha. Jarida la Uhispania Mundo Deportivo limeripoti kwamba Barcelona, ​​ambayo hivi karibuni iliwaongeza mikataba Pedri, Gavi, Pau Cubarsi, Ronald Araujo na Inigo Martinez, wanapanga kuweka masharti mapya kwa Yamal, Jules Kounde na Raphinha, huku Wachezaji hao wakiwa tayari wamepewa ofa mezani.

Mkataba wa sasa wa Raphinha unajumuisha kifungu cha ununuzi cha €1bn, ingawa thamani hiyo inaweza kushuka kwa siku zijazo.

Fainali za Kombe la Dunia 2026, zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada, zimetajwa kuwa muda mwafaka wa kuachana naye na kumpa Raphinha kandarasi mpya kipindi kilichosalia cha msimu huu na ujao ili kutimiza malengo yake ya kutwaa taji akiwa na Barcelona kuliko kuondoka akiwa huru.