
Daniel Dubois - Bondia wa Nchini Uingereza
Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 27 anayemiliki mkanda wa IBF hapo jana alikosekana katika mkutano wa wanahabari na baadaye akafanyiwa vipimo na kugundulika kuwa hatoweza kupambana katika pambano hilo
Kwa sasa Parker raia wa New Zealand mwenye umri wa miaka 33 atapambana na Mkongo Martin Bakole ambaye ameteuliwa kama mbadala wa Dubois anayeumwa .
Haijaelezwa bayana ni nini hasa kinacho msibu Dubois ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kutetea taji lake la IBF kwa mara ya pili.