Alhamisi , 20th Feb , 2025

Mmiliki wa recording label ya Bad Nation Omary Mwanga maarufu kama Marioo ameweka wazi matamanio yake makubwa ya kutaka kufunga ndoa siku za hivi karibuni

Pichani ni Marioo na Paula

Marioo ameeleza hayo baada ya kuhudhuria katika harusi ya marafiki zao Hamisa Mobeto  pamoja na Mchezaji mpira wa klabu ya Yanga mwenye asili ya Bukinafaso Aziz Ki

Marioo ameweka wazi matamanio yake hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo amepost video akiwa na mpenzi wake na kisha kuandika.....''Nimepata Mshawasha wa kuoa Wallah'' jambo ambalo limewaaminisha mashabiki wa watu hawa Marioo na Paula kuwa huenda wakakutana ndoa siku za hivi karibuni