Alhamisi , 19th Dec , 2024

Prisons chini ya Kocha Makata imecheza michezo 14 ya Ligi Kuu na kushinda michezo 2, droo 5, kupoteza 7 huku ikifunga magoli 6 na kuruhusu magoli 13 inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu.

Klabu ya Tanzania Prisons kutoka Mkoani Mbeya imeachana na Kocha Mkuu Mbwana Makata pamoja na Msaidiz wake Renatus Shija kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo.

Aidha Klabu hiyo pia imeachana na Afisa habari wake Bright Mbwilo ambaye amehudumu kwa muda wa miezi miezi 3 pekee tangu atangazwe kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Waisaka Chacha aliyehudumu kwa muda mwaka mmoja pekee.

Kikosi cha Wajelajela kipo Dar es Salaam kikijiandaa kukabiliana na Yanga SC kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara utakaochezwa Disemba 22 Uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.

Timu hiyo yenye makao yake makuu mkoani Mbeya imeshiriki kwa muda mrefu ligi kuu bila kushuka mwenendu wa msimu hii ni mbovu zaidi kwa timu hiyo tangu ipande daraja tena kucheza ligi kuu Tanzania bara baada ya kushuka msimu wa 2009.

Tanzania Prisons ilipanda kucheza tena ligi kuu msimu wa 2011 baada ya nyakati mbaya ilizowahi kuzipitia timu hiyo haikufanya usajili ambao ungeweza kuisaidia kutokana na kutokumaliza vizuri msimu uliopita. 

Kikosi hiko kinapitia wakati mgumu kutokana na Wachezaji wake nyota kutokuwa kwenye wakati mzuri msimuu huu.Washambuliaji wake Jeremiah Juma na Samson Mbangula wanahangaika kutafuta viwango vyao na kusababisha timu kukosa kufunga magoli ya kutosha.

Maingizo mapya yanategemewa kwenye dirisha hili dogo ili kuiimarisha timu hiyo kama inataka kusalia kucheza ligi kuu msimu ujao.